Ufunuo 22 — Mto wa Uzima
Ufunuo 22 — Mto wa Uzima
[Verse] Katikati ya njia kuu yake, na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. [Chorus] Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake, na watumwa wake watamtumikia. Nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. [Verse] Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele. Kisha akaniambia: Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.