Mto wa Uzima

Mto wa Uzima

[Verse 1]
Katikati ya njia kuu yake, na upande huu na upande huu wa ule mto,
ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili,
wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

[Verse 2]
Wala hapatakuwa na laana yoyote tena.
Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake, na watumwa wake watamtumikia.
Nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.

[Verse 3]
Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua;
kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.

[Verse 4]
Kisha akaniambia: Maneno haya ni amini na kweli.
Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.
Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.